TIMU YA ULINZI NA USALAMA WA MTOTO HALMASHAURI WILAYA YA MBEYA
Utangulizi
Halmashauri ya wilaya ya mbeya ni
miongoni mwa Halmashauri kumi (10) zinazounda mkoa wa mbeya. Halmashauri ya
wilaya ya mbeya ina jumla ya tarafa tatu zenye kata 28
Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 inaonesha kuwa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya ina jumla ya watu 305,319 ambao kati yao watoto wenye umri chini ya miaka kumi na nane ni 158,688 sawa na asilimia hamsini na mbili (52%) ya watu wote. Halmashauri ya wilaya ya Mbeya inajukumu la kuhakikisha kuwa watu wake wanaishi katika mazingira mazuri kwa kuzingatia ustawi wa jamii. Takwimu zinaonesha kuwa matukio ya unyanyasaji na ukatili dhidi ya mtoto yanaongezeka siku hadi siku. Ili kuhakikisha matukio hayo yanatokomezwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imechukua hatua mbalimbali ikiwa ni kutunga sera na sheria zinazohakikisha ulinzi na usalama wa mtoto. Sera na sheria hizo ni kama vile sheria ya mtoto ya mwaka 2009, sera ya maendeleo ya mtoto ya mwaka 2008, sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2015, sera ya taifa ajira na sheria ya mahusiano ya mwaka 2004, sharia maalum ya makosa ya kujamiiana ya mwaka 1998, sheria ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010, na sheria ya kupinga usafirishaji haramu wa binadamu ya mwaka 2008. Sheria na sera hizo zimetungwa ili kuhakikisha mtoto analindwa na kupatiwa haki zake stahiki za kuishi na kuendelezwa.
Pamoja na sera na sheria hizo pia Serikali imesaini mikataba ya kimataifa yenye lengo la kumlinda mtoto kama vile “The United Nations Convention on the Rights of the Child” na “The African Charter on the Rights and Welfare of the Child”.
Sambamba na
hili Serikali kupitia wizara ya Afya na Ustawi wa jamii ikishirikiana na
Shirika la Kimataifa la Mfuko wa Watoto (UNICEF) imeazimia kila Halmashauri iwe
na timu ya ulinzi na usalama wa mtoto kwa lengo la kuhakikisha mtoto analindwa
na kupatiwa haki zake stahiki kuanzia ngazi ya chini. Novemba 2013 Halmashauri
ya Wilaya ya Mbeya ilianzisha timu ya ulinzi na usalama wa mtoto. Timu hii
inajumuisha wadau mbalimbali toka asasi za kiserikali na zisizo za kiserikali.
Timu inajumla ya wajumbe thelathini (30) wa kada mbalimbali ambazo ni Afya,
Sheria, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Habari, Polisi kitengo cha pollisi
jamii, Magereza, Idara ya majaribio na huduma kwa jamii, Mahakama, Mipango,
Asasi za kiraia na Viongozi wa dini madhehebu ya Kiislama na Kikristo. Wajumbe hao
pamoja na nafasi zao katika timu ni kama ifuatavyo:
SN
|
JINA
|
NAFASI/CHEO
|
1
|
Magdalena Songoma
|
Mwenyekiti
|
2
|
Tobias Mwalwego
|
Katibu
|
3
|
Dr. Louis Chomboko
|
Mjumbe
|
4
|
Peter L. Mushali
|
Mjumbe
|
5
|
Rose Rweyemamu
|
Mjumbe
|
6
|
Emiliana Mdemu
|
Mjumbe
|
7
|
Mathiasi Kajigili
|
Mjumbe
|
8
|
Mary Gumbo
|
Mjumbe
|
9
|
Emmiliana Mbise
|
Mjumbe
|
10
|
Pudensiana Baitu
|
Mjumbe
|
11
|
Mery Patrick
|
Mjumbe
|
12
|
Marietha Mlozi
|
Mjumbe
|
13
|
Kaliana Tulyanje
|
Mjumbe
|
14
|
Dolorosa Samky
|
Mjumbe
|
15
|
Mustafa Mjema
|
Mjumbe
|
16
|
A.S Mwandiga
|
Mjumbe
|
17
|
Happiness A. Chuwa
|
Mjumbe
|
18
|
Ester Castory
|
Mjumbe
|
19
|
Wilfred Kasambala
|
Mjumbe
|
20
|
Bevarine Mgoda
|
Mjumbe
|
21
|
Elizabeth Lyombe
|
Mjumbe
|
22
|
Dr. Robert Mbinda
|
Mjumbe
|
23
|
Emiliana Komba
|
Mjumbe
|
24
|
Darius Limandola
|
Mjumbe
|
25
|
Sikudhani Khamisi
|
Mjumbe
|
26
|
Annuciatha Christian
|
Mjumbe
|
27
|
Grolia
|
Mjumbe
|
28
|
Rhoda Ngole
|
Mjumbe
|
29
|
Lilian Kilongumtwa
|
Mjumbe
|
30
|
Hamza Mwangomale
|
Mjumbe
|
Muundo wa timu
Timu ya
Ulinzi na Usalama wa Mtoto inafanya kazi kuanzia ngazi ya chini, yaani ngazi ya
Kijiji, Kata na Wilaya kama inavyooneshwa kwenye chati hapo chini.
tunaomba taarifa ya kesi ambazo zimefikishwa mahakamani,zilizotolewa maamuzi,ambazo bado kutolewa hukumu.aina ya kesi mfano ubakaji,ukatili nk.
ReplyDelete