Tuesday, 7 March 2017

TIMU YA ULINZI NA USALAMA WA MTOTO HALMASHAURI YA WILAYA YA MBEYA YAPITISHA KATIBA YA KUANZISHA MFUKO WA KUSAIDIA WATOTO NA WANAWAKE

Timu ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya (Mbeya DCPT) imefanya kikao cha robo ya pili ya mwaka kwa ajili ya kujadili shughuli mbalimbali zilizotekelezwa na timu hiyo kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba. Akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa Mbeya DCPT Bi Magdalena Songoma alisema kuwa kikao hicho ni cha kawaida kwa ajili ya kujadili shughuli za utekelezaji wa timu pamoja na masuala mbalimbali yanayowahusu watoto katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.

Baadhi ya wajumbe wa Mbeya DCPT wakiwa kwenye kikao kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi za Idara ya Maji Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya

Licha ya kujadili shughuli za utekelezaji kikao hicho kilijadili pia katiba ya kuanzisha mfuko wa kusaidia watoto waliokubwa na matukio ya unyanyasaji. Akielezea Umuhimu wa mfuko huo Mwenyekiti wa Timu Bi Songoma amesema kuwa timu hiyo inakabiliana na changamoto za kifedha pale wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku haswa wanapomuhudumia mtoto anayetoka katika familia yenye hali ngumu ya kiuchumi. Kutokana na changamoto hiyo ndio ikawapelekea kuanzisha mfuko huo utakao kuwa unakusanya fedha toka kwa wanatimu pamoja na wadau mbalimbali kwa sababu timu hiyo haina chanzo kingine cha mapato.

"Tumekuwa tukikabiliana na changamoto nyingi katika kutekeleza majukumu yetu ya kila siku, lakini changamoto kubwa kwetu ni uhaba wa fedha haswa tunapomuhudumia mtoto anayetoka katika familia ya kimasikini. Unajua sisi tunafanya kazi vijijini ambapo wananchi wetu wengi ni masikini, utakuta mzazi ama mlezi anashidwa kumnunulia mtoto vifaa vya shule kama vile sare, madaftari na kalamu hali inayopelekea watoto wengi kushindwa kuendelea na masomo"

"Tukikutana na mazingira kama hayo inatupasa kutoa pesa zetu mfukoni lakini si kila wakati mtu unakua na pesa mfukoni na tunapoliwasilisha Halmashauri tunaambiwa kuwa Halmashauri haina bajeti hiyo. hivyo sasa sisi kama timu tumeona kunaumuhimu wa kuanzisha huu mfuko kwa ajili ya kukabiliana na changamoto hiyo" Alisema Songoma.

Akizungumza katika kikao hicho mwakilishi wa UNICEF Tanzania Ndg. Joseph Matibwi alisema anawapongeza sana wanatimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kuwa na wazo zuri ambalo linalenga kukabiliana na changamoto hiyo. lakini pia aliwaambia kuwa kwa sasa Timu za Ulinzi na Usalama wa Mtoto zitaongezewa jukumu lingine la kushughulikia wanawake hivyo timu hizo zitabadilika na kuitwa "Protection Committee" Akashauri ili kuendana na mabadiliko hayo ni vyema mfuko huo usiitwe (MFUKO WA KUSAIDIA WATOTO MBEYA DCPT) bali uitwe (MFUKO WA KUSAIDIA WATOTO NA WANAWAKE MBEYA PROTECTION COMMITTEE)

Ndg. Joseph Matibwi Mwakilishi wa UNICEF Tanzania akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa Timu ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya


 

No comments:

Post a Comment