Wajumbe wa Kamati za Ulinzi na Usalama wa Mtoto ngazi za Vijiji wakimsikiliza kwa makini muwezeshaji (hayupo pichani) wa mafunzo ya timu hizo
Timu ya Ulinzi na
usalama wa mtoto Wilaya ya Mbeya imeendesha mafunzo ya siku tatu kuanzia tarehe
29/03/2016 hadi 31/03/2016 kwa vijiji 41 vya Wilaya hiyo. Mwenyekiti wa timu ya
Ulinzi na usalama wa mtoto ya Wilaya ambaye pia
ni Afisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya, Bi Magdalena Songoma amesema kuwa mafunzo
hayo yanatolewa kwa Timu za Ulinzi na Usalama wa Mtoto ngazi za vijiji kwa
ajili ya kuwajengea uwezo katika kufanya kazi za kuibua na kuwasaidia watoto
wanaonyanyaswa na kufanyiwa vitendo vya kikatili.
“Mafunzo haya
yanatolewa kwa Kamati zetu za ngazi za vijiji za kuwahudumia watoto walio
katika mazingira hatarishi ambazo pia ni timu za ulinzi za mtoto ngazi za
vijiji kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kufanya kazi katika kushughulikia
matatizo mbalimbali yanayowakabili watoto. Kimsingi watoto wengi waishio vijijini
wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ya unyanyasaji na ukatili lakini matukio
hayo hayaripotiwi katika ngazi husika na matokeo yake wanayamalila kifamilila
bila ya kuzingatia haki stahiki za mtoto. Hivyo timu hizo zinapewa mafunzo hayo
kwaajili ya kujua mbinu na kanuni za kuzifuata pale wanapoona mtoto katika
kijiji walichopo anafayiwa vitendo kama hivyo”
Bi Songoma, amesema
kuwa vijiji hivyo vinavyopata mafunzo vimetoka katika kata nane ambazo ni Isuto,
Itawa, Ikukwa, Mjele, Santilya, Ilungu, Lwanjilo, na Maendeleo. Na katika kata
hizo vijiji vilivyopewa mafunzo hayo ni Isuto vijiijii vilivyopewa mafunzo ni Iwowo,
Pansungu, Igalukwa, Shigamba, Isuto, Itete, Mlowo, Shitete, Shizingo kata ya
Isuto. Vijiji vingine ni kijiji cha Itawa kata ya Itawa, Mjele kata ya
Mjele, Ikukwa na Simboya kata ya Ikukwa
na vijiji vya Itizi, Isongole, Sanje, Ruanda, Nsheha, Santilya, Mpande, Iswago,
Jojo, na Masyeta kata ya Santilya. Pia kata ya Ilungu vijiji vilivyopewa mafunzo
ni Mashese, Ngole, Ifupa, Kikondo, Mwela, nyalwela, na Shongo. Na kata ya
Lwanjilo ni vijiji vya Lwanjilo na Ilowelo na kata ya Maendeleo ni vijiji vya
Ikoho, Itambalila, Isebe, Usoha, Muungano na Izumbwe.
Amosi W. Mwakalyalya
Mwenyekkiti wa kijiji cha Shisonta kata ya Isuto amesema kuwa amefarijika na
mafunzo hayo waliopewa kwa sababu yamewajengea uwezo na mbinu mpya za kugundua
na kushughulikia vitendo mbalimbali vya ukatili wanaofanyiwa watoto kwa sababu
vitendo hivyo vimeshamiri sana katika jamii yao. “Kiukweli tunawashukuru sana
wawezeshaji kwa mafuzo waliotupa kwa sababu yametupatia mbinu mpya ukizingatia
kwamba tangu kamati hiyo iundwe kijii kwetu hatukuwahi kupata mafunzo yoyote.
Lakini pia katika jamii yetu vitendo vya unyanyasaji na ukatili vimeenea sana
kijijini kwetu lakini tulikua tunashidwa kuchukua hatua yoyote kwasababu
tulikua hatujui tuanzie wapi, lakini mafunzo haya yametufungu na kutupa njia za
kufuata”
Pia mwenyekiti huyo wa
kijiji ameahidi kuwa watayafanyia kazi mafunzo yote waliopewa na kuongeza kuwa
watakua wajumbe kwa jamii nzima na kuwapatia elimu waliopewa ili vitendo vya
unyanyasaji na ukatili viweze kupungua katika vijiji vyao.
MATOKEO
YAANZA KUONEKANA
TUKIO
LA MTOTO KUBAKWA KIJIJI CHA MLOWO
Ni siku ya mwisho ya
mafunzo ya ulinzi wa mtoto, afisa mtendaji wa kijiji cha mlowo ameripotiwa
tukio la mtoto mdogo kubakwa na watuhumiwa kukamatwa na kufikishwa kwenye
vyombo vya sheria.
No comments:
Post a Comment