Tuesday, 7 March 2017

TIMU YA ULINZI NA USALAMA WA MTOTO HALMASHAURI YA WILAYA YA MBEYA YAPITISHA KATIBA YA KUANZISHA MFUKO WA KUSAIDIA WATOTO NA WANAWAKE

Timu ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya (Mbeya DCPT) imefanya kikao cha robo ya pili ya mwaka kwa ajili ya kujadili shughuli mbalimbali zilizotekelezwa na timu hiyo kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba. Akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa Mbeya DCPT Bi Magdalena Songoma alisema kuwa kikao hicho ni cha kawaida kwa ajili ya kujadili shughuli za utekelezaji wa timu pamoja na masuala mbalimbali yanayowahusu watoto katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.

Baadhi ya wajumbe wa Mbeya DCPT wakiwa kwenye kikao kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi za Idara ya Maji Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya

Licha ya kujadili shughuli za utekelezaji kikao hicho kilijadili pia katiba ya kuanzisha mfuko wa kusaidia watoto waliokubwa na matukio ya unyanyasaji. Akielezea Umuhimu wa mfuko huo Mwenyekiti wa Timu Bi Songoma amesema kuwa timu hiyo inakabiliana na changamoto za kifedha pale wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku haswa wanapomuhudumia mtoto anayetoka katika familia yenye hali ngumu ya kiuchumi. Kutokana na changamoto hiyo ndio ikawapelekea kuanzisha mfuko huo utakao kuwa unakusanya fedha toka kwa wanatimu pamoja na wadau mbalimbali kwa sababu timu hiyo haina chanzo kingine cha mapato.

"Tumekuwa tukikabiliana na changamoto nyingi katika kutekeleza majukumu yetu ya kila siku, lakini changamoto kubwa kwetu ni uhaba wa fedha haswa tunapomuhudumia mtoto anayetoka katika familia ya kimasikini. Unajua sisi tunafanya kazi vijijini ambapo wananchi wetu wengi ni masikini, utakuta mzazi ama mlezi anashidwa kumnunulia mtoto vifaa vya shule kama vile sare, madaftari na kalamu hali inayopelekea watoto wengi kushindwa kuendelea na masomo"

"Tukikutana na mazingira kama hayo inatupasa kutoa pesa zetu mfukoni lakini si kila wakati mtu unakua na pesa mfukoni na tunapoliwasilisha Halmashauri tunaambiwa kuwa Halmashauri haina bajeti hiyo. hivyo sasa sisi kama timu tumeona kunaumuhimu wa kuanzisha huu mfuko kwa ajili ya kukabiliana na changamoto hiyo" Alisema Songoma.

Akizungumza katika kikao hicho mwakilishi wa UNICEF Tanzania Ndg. Joseph Matibwi alisema anawapongeza sana wanatimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kuwa na wazo zuri ambalo linalenga kukabiliana na changamoto hiyo. lakini pia aliwaambia kuwa kwa sasa Timu za Ulinzi na Usalama wa Mtoto zitaongezewa jukumu lingine la kushughulikia wanawake hivyo timu hizo zitabadilika na kuitwa "Protection Committee" Akashauri ili kuendana na mabadiliko hayo ni vyema mfuko huo usiitwe (MFUKO WA KUSAIDIA WATOTO MBEYA DCPT) bali uitwe (MFUKO WA KUSAIDIA WATOTO NA WANAWAKE MBEYA PROTECTION COMMITTEE)

Ndg. Joseph Matibwi Mwakilishi wa UNICEF Tanzania akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa Timu ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya


 

Monday, 11 April 2016

TIMU YA ULINZI NA USALAMA WA MTOTO WILAYA YA MBEYA YAENDESHA MAFUNZO KWA VIJIJI 41

Mjumbe wa Timu ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto ngazi ya Wilaya akitoa mafunzo kwa Kamati za Ulinzi na Usalama wa Mtoto ngazi za Vijijini Wilaya ya Mbeya.

Wajumbe wa Kamati za Ulinzi na Usalama wa Mtoto ngazi za Vijiji wakimsikiliza kwa makini muwezeshaji (hayupo pichani) wa mafunzo ya timu hizo


Timu ya Ulinzi na usalama wa mtoto Wilaya ya Mbeya imeendesha mafunzo ya siku tatu kuanzia tarehe 29/03/2016 hadi 31/03/2016 kwa vijiji 41 vya Wilaya hiyo. Mwenyekiti wa timu ya Ulinzi na usalama wa mtoto ya Wilaya ambaye pia  ni Afisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya, Bi Magdalena Songoma amesema kuwa mafunzo hayo yanatolewa kwa Timu za Ulinzi na Usalama wa Mtoto ngazi za vijiji kwa ajili ya kuwajengea uwezo katika kufanya kazi za kuibua na kuwasaidia watoto wanaonyanyaswa na kufanyiwa vitendo vya kikatili.

“Mafunzo haya yanatolewa kwa Kamati zetu za ngazi za vijiji za kuwahudumia watoto walio katika mazingira hatarishi ambazo pia ni timu za ulinzi za mtoto ngazi za vijiji kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kufanya kazi katika kushughulikia matatizo mbalimbali yanayowakabili watoto.  Kimsingi watoto wengi waishio vijijini wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ya unyanyasaji na ukatili lakini matukio hayo hayaripotiwi katika ngazi husika na matokeo yake wanayamalila kifamilila bila ya kuzingatia haki stahiki za mtoto. Hivyo timu hizo zinapewa mafunzo hayo kwaajili ya kujua mbinu na kanuni za kuzifuata pale wanapoona mtoto katika kijiji walichopo anafayiwa vitendo kama hivyo”

Bi Songoma, amesema kuwa vijiji hivyo vinavyopata mafunzo vimetoka katika kata nane ambazo ni Isuto, Itawa, Ikukwa, Mjele, Santilya, Ilungu, Lwanjilo, na Maendeleo. Na katika kata hizo vijiji vilivyopewa mafunzo hayo ni Isuto vijiijii vilivyopewa mafunzo ni Iwowo, Pansungu, Igalukwa, Shigamba, Isuto, Itete, Mlowo, Shitete, Shizingo kata ya Isuto. Vijiji vingine ni kijiji cha Itawa kata ya Itawa, Mjele kata ya Mjele,  Ikukwa na Simboya kata ya Ikukwa na vijiji vya Itizi, Isongole, Sanje, Ruanda, Nsheha, Santilya, Mpande, Iswago, Jojo, na Masyeta kata ya Santilya. Pia kata ya Ilungu vijiji vilivyopewa mafunzo ni Mashese, Ngole, Ifupa, Kikondo, Mwela, nyalwela, na Shongo. Na kata ya Lwanjilo ni vijiji vya Lwanjilo na Ilowelo na kata ya Maendeleo ni vijiji vya Ikoho, Itambalila, Isebe, Usoha, Muungano na Izumbwe.

Amosi W. Mwakalyalya Mwenyekkiti wa kijiji cha Shisonta kata ya Isuto amesema kuwa amefarijika na mafunzo hayo waliopewa kwa sababu yamewajengea uwezo na mbinu mpya za kugundua na kushughulikia vitendo mbalimbali vya ukatili wanaofanyiwa watoto kwa sababu vitendo hivyo vimeshamiri sana katika jamii yao. “Kiukweli tunawashukuru sana wawezeshaji kwa mafuzo waliotupa kwa sababu yametupatia mbinu mpya ukizingatia kwamba tangu kamati hiyo iundwe kijii kwetu hatukuwahi kupata mafunzo yoyote. Lakini pia katika jamii yetu vitendo vya unyanyasaji na ukatili vimeenea sana kijijini kwetu lakini tulikua tunashidwa kuchukua hatua yoyote kwasababu tulikua hatujui tuanzie wapi, lakini mafunzo haya yametufungu na kutupa njia za kufuata”

Pia mwenyekiti huyo wa kijiji ameahidi kuwa watayafanyia kazi mafunzo yote waliopewa na kuongeza kuwa watakua wajumbe kwa jamii nzima na kuwapatia elimu waliopewa ili vitendo vya unyanyasaji na ukatili viweze kupungua katika vijiji vyao.
MATOKEO YAANZA KUONEKANA
TUKIO LA MTOTO KUBAKWA KIJIJI CHA MLOWO
Ni siku ya mwisho ya mafunzo ya ulinzi wa mtoto, afisa mtendaji wa kijiji cha mlowo ameripotiwa tukio la mtoto mdogo kubakwa na watuhumiwa kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Tuesday, 1 March 2016


TIMU YA ULINZI NA USALAMA WA MTOTO HALMASHAURI WILAYA YA MBEYA

Utangulizi
Halmashauri ya wilaya ya mbeya ni miongoni mwa Halmashauri kumi (10) zinazounda mkoa wa mbeya. Halmashauri ya wilaya ya mbeya ina jumla ya tarafa tatu zenye kata 28

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 inaonesha kuwa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya ina jumla ya watu 305,319 ambao kati yao watoto wenye umri chini ya miaka kumi na nane ni 158,688 sawa na asilimia hamsini na mbili (52%) ya watu wote. Halmashauri ya wilaya ya Mbeya inajukumu la kuhakikisha kuwa watu wake wanaishi katika mazingira mazuri kwa kuzingatia ustawi wa jamii. Takwimu zinaonesha kuwa matukio ya unyanyasaji na ukatili dhidi ya mtoto yanaongezeka siku hadi siku. Ili kuhakikisha matukio hayo yanatokomezwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imechukua hatua mbalimbali ikiwa ni kutunga sera na sheria zinazohakikisha ulinzi na usalama wa mtoto. Sera na sheria hizo ni kama vile sheria ya mtoto ya mwaka 2009, sera ya maendeleo ya mtoto ya mwaka 2008, sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2015, sera ya taifa ajira na sheria ya mahusiano ya mwaka 2004, sharia maalum ya makosa ya kujamiiana ya mwaka 1998, sheria ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010, na sheria ya kupinga usafirishaji haramu wa binadamu ya mwaka 2008. Sheria na sera hizo zimetungwa ili kuhakikisha mtoto analindwa na kupatiwa haki zake stahiki za kuishi na kuendelezwa.

Pamoja na sera na sheria hizo pia Serikali imesaini mikataba ya kimataifa yenye lengo la kumlinda mtoto kama vile “The United Nations Convention on the Rights of the Child” na “The African Charter on the Rights and Welfare of the Child”.  
Sambamba na hili Serikali kupitia wizara ya Afya na Ustawi wa jamii ikishirikiana na Shirika la Kimataifa la Mfuko wa Watoto (UNICEF) imeazimia kila Halmashauri iwe na timu ya ulinzi na usalama wa mtoto kwa lengo la kuhakikisha mtoto analindwa na kupatiwa haki zake stahiki kuanzia ngazi ya chini. Novemba 2013 Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ilianzisha timu ya ulinzi na usalama wa mtoto. Timu hii inajumuisha wadau mbalimbali toka asasi za kiserikali na zisizo za kiserikali. Timu inajumla ya wajumbe thelathini (30) wa kada mbalimbali ambazo ni Afya, Sheria, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Habari, Polisi kitengo cha pollisi jamii, Magereza, Idara ya majaribio na huduma kwa jamii, Mahakama, Mipango, Asasi za kiraia na Viongozi wa dini madhehebu ya Kiislama na Kikristo. Wajumbe hao pamoja na nafasi zao katika timu ni kama ifuatavyo:
SN
JINA
NAFASI/CHEO
1
Magdalena Songoma
Mwenyekiti
2
Tobias Mwalwego
Katibu
3
Dr. Louis Chomboko
Mjumbe
4
Peter L. Mushali
Mjumbe
5
Rose Rweyemamu
Mjumbe
6
Emiliana Mdemu
Mjumbe
7
Mathiasi Kajigili
Mjumbe
8
Mary Gumbo
Mjumbe
9
Emmiliana Mbise
Mjumbe
10
Pudensiana Baitu
Mjumbe
11
Mery Patrick
Mjumbe
12
Marietha Mlozi
Mjumbe
13
Kaliana Tulyanje
Mjumbe
14
Dolorosa Samky
Mjumbe
15
Mustafa Mjema
Mjumbe
16
A.S Mwandiga
Mjumbe
17
Happiness A. Chuwa
Mjumbe
18
Ester Castory
Mjumbe
19
Wilfred Kasambala
Mjumbe
20
Bevarine Mgoda
Mjumbe
21
Elizabeth Lyombe
Mjumbe
22
Dr. Robert Mbinda
Mjumbe
23
Emiliana Komba
Mjumbe
24
Darius Limandola
Mjumbe
25
Sikudhani Khamisi
Mjumbe
26
Annuciatha Christian
Mjumbe
27
Grolia
Mjumbe
28
Rhoda Ngole
Mjumbe
29
Lilian Kilongumtwa
Mjumbe
30
Hamza Mwangomale
Mjumbe

Muundo wa timu
Timu ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto inafanya kazi kuanzia ngazi ya chini, yaani ngazi ya Kijiji, Kata na Wilaya kama inavyooneshwa kwenye chati hapo chini.